Fani
katika Ushairi wa Malenga Wapya
Hakiki Fani katika Ushairi wa Malenga Wapya
MWANDISHI: TAASISI YA KISWAHILI, ZANZIBAR
WACHAPISHAJI: OXFORD UNIVERSITY PRESS
MWAKA: 2001
JINA LA KITABU
Jina la kitabu linasadifu yaliyomo katika kitabu. Kwa upande wa
maudhui mambo yanayoelezwa mengi yanaigusa jamii ya sasa. Masuala ya maadili,
siasa, uchumi, ukombozi wa kiutamaduni changamoto na suluhisho ya matatizo
yanayoikumba jamii yanaendana na wakati wa sasa. Hivyo upya wa malenga wapya ni
kweli. Kifani pia Malenga wapya wameweka muundo na mtindo wa kisasa.
MUUNDO
Tunapohakiki muundo katika ushairi tunaangalia idadi ya mistari
katika ubeti. Ubeti huweza kuwa na mistari miwili, mitatu, minne na kuendelea. Aina
za muundo zimepewa istilahi maalum kuutofautisha aina moja na nyingine mfano
mashiri yenye mistari miwili katika ubeti ni Tathnia. Imetumika miundo
tofautitofauti katika diwani hii. Mfano:
Tathlitha
Haya ni mashairi ambayo yana mistari mitatu kwa kila beti, mengi
ya mashairi haya ni ya kisasa. Mfano ni shairi la“Hali halisi”, “Puuzo”, “Ua”, “Kuunge”, “Tunzo”.
Tarbia
Haya ni mashairi yenye mistari mine. Mfano ni shairi la“Kitendawili”, “Mkulima”, “Majonzi”, “Bahari”, “Samaki mtungoni”
“Kifungo”,na mengine mengi.
Takhmisa
Haya huwa na muundo wa mistari mitano katika kila ubeti. Mfano
ni mashairi ya“Siharakie maisha”, na
“Israfu”.
Sabilia
Haya ni mashairi yenye mistari kuanzia sita na kuendelea. Mfano
ni shairi la“Punda”na “Pasua uwape
ukweli”
MTINDO
Imetumika mitindo ya aina zote mbili. Kwanza wametumia mtindo wa
kisasa. Huu ni mtindo ambao haufuati kanuni za urari wa vina na mizani katika
beti pia huitwa mashairi huru. Mtindo mwingine ni mtindo wa kimapokeo, huu
hufuata kanuni na sheria zote za vina na mizani katika utunzi wake. Mara nyingi
huwa na mistari minne katika kila ubeti.
Mfano wa mashairi yaliyotumia mtindo wa kisasa ni mashairi ya“Pasua uwape ukweli”, “Haki”. “Payuka”. Mfano shairi la Pasua
uwape ukweli
Pia mfano wa mashairi ya kimapokeo ni shairi la“Mkulima”, “Bahari”, “Tuyazingatie haya” “Nipate wapi mwingine”.
MATUMIZI YA LUGHA
Diwani ya malenga wapya imetumia lugha yenye ubunifu bora wa
kisanaa.Vilevile ni lugha rahisi na sanifu inayoeleweka kwa hadhira lengwa.
TAMATHALI
ZA SEMI
·
Tashibiha:“Nizikwe kama wezangu, nisitupwe kama paka” -Shairi
la“Nini wanangu”.“Hata
pamoja muweko, ubaguzi umezama,kama nguzo” -Shairi
la“Tunzo ubeti wa
nne”.“Mfanowe kama radi, chini inapoanguka”.-Shairi
la“Nipate wapi
mwingine”.“Nikabaki kama ng’onda” -Shairi
la“Nipatieni dawa”.“Maisha
ni kama njia”-Shairi la“Maisha ni kama njia”.“Yameotewa na kombe, mithili gome la mti”-Shairi
la“Bahari ubeti wa pili”.
·
Tashihisi:“Ewe ulimi sikia” -Shairi la“Ulimi”.“Haki wa tutisha,tusikuandame,kwa matendo yetu” –Shairi la“Haki ubeti wa kwanza”.“Njiwa ameishanitoka, nipate wapi
mwingine”-Shairi la“Nipate
wapi mwingine”.“Samaki wasikitika, kudai walikotoka, Wote wamekasirika,
uhuru wanachotaka,”-Shairi la“samaki mtungoni”.
·
Sitiari:“wamejipa uwezo wa Rabuka” – “Mpaka lini”“Paka shume jigeuza” –
“Kwanini?”“mshumaa ” – “Hali halisi”Mbinu
nyingine za kisanaa.
·
Onomatopea/
tanakali sauti:“kokoriko”-
“Mkulima”“Parakacha” – “kwanini”.
·
Takriri:“Charuka” – “charuka”
·
Tashititi:“Nasikia mnatunga mwatungani washairi?” “mwabwaja mwasema nini”Matumizi
ya semi
·
Methali:“Simwamshe asilani aliyelala usingizini” – “Payuka”“Fahali
wapiganapo, nyasi ndio huumia”- “Sokomoko baharini”“Subira yavuta heri”-
“Siharakie maisha”
·
Taswira:Matumizi
ya taswira“Samaki” – wanyonge –
“samaki mtungoni”“Ua” – mpenzi – “Ua”“Punda”-wanyonge – “Punda”“Mvuvi” –
wanyonyaji – “Samaki mtungoni”“Njiwa” – mpenzi – “Nipate wapi
mwingine”“Baharini” – nchi – “Sokomoko”;“Abiria”- wananchi –“Sokomoko”