VIUMBE HAI
Muundo na sifa za viumbe hai
Seli
Seli ni
kiini cha msingi wa kiumbe hai.seli ni vitengo vya msingi vya uhai.
Mfano
seli ya mimea,seli ya wanyama,seli ya bakteria nk
Aina za seli
I.
Prokarioti
II.
Eukarioti
Prokarioti
ni aina ya seli ambayo haina utando wa nyukilia/kiini
Mf.seli
ya bakteria
Eukarioti ni aina ya seli yenye utando wa
nyukilia/kiini.mf seli ya mnyama na seli ya mmea
Muundo wa seli za mnyama na mmea
Seli
huundwa na sitoplazimu,kiwambo cha seli,nyukilia,vakuoli,kloroplasti na ukuta
wa seli.kloroplasti na ukuta wa seli zipo kwenye seli yam mea tu.
sehemu ya seli
|
kazi
|
1.sitoplazimu
Ø Ni
kimiminiko kizito
Ø Nyukilia,vakuoli
na kloroplasti huelea katika sitoplazimu
|
·
Hutumika kama makazi ya
nyukilia,vakuoli na kloroplasti
·
Mabadiliko ya kikemikali hutokea
kwenye sitoplazimu
|
2.kiwambo
cha seli
Ni
kiwambo ambacho kimezunguka sitoplazimu kwa nje
|
·
Huruhusu vitu kuingia na kutoka
kwenye seli.mf hewa,maji,vyakula na taka mwili
|
3.nyukilia
Imezungukwa
na sitoplazimu (kiwambo cha nyukilia).
|
·
Hutawala na kuratibu shughuli
zote za seli
|
4.vakuoli
Zina
myeyuko angavu
|
·
Hutunza maji kwa mmea
·
Hutunza chakula
·
Husafirisha taka mwili kutoka
kwenye seli
|
5.kloroplasti
Ni
chembe ndogo sana zenye klorofili.klorofili huwa na rangi ya kijani ambazo hunasa
mwanga wa jua ili kutengeneza chakula chake katika kloroplasti.
6.ukuta
wa seli
|
·
Kutengeneza chakula cha mmea
·
Huzunguka seli ya mmea kwa nje
·
Kazihuipa seli umbo maalumu
·
Hulinda seli
|
Tofauti ya muundo kati ya seli ya
mnyama na seli yam mea
Seli
ya mnyama
|
Seli
ya mmea
|
I.
Haina ukuta wa seli
II.
Haina kloroplasti
III.
Ina vakuoli ndogo sana nay a muda
mfupi
IV.
Haina umbo maalumu
|
Ina ukuta wa seli
Ina kloroplasti
Ina vakuoli kubwa ya kudumu
Ina umbo maalumu
|
Viumbe hai
Ø Ni
vitu vinavyoonesha tabia na sifa zote za uhai kwa kiumbe.mf.
binadamu,bakteria,mimea nk
Sifa za viumbe hai
1.
Huzaa na kuongezeka idadi
2.
Hujongea
3.
Hula chakula
4.
Hutoa taka mwili
5.
Hupumua
6.
Huhisi mabadiliko katika mazingira
7.
Hukua au kuongezeka kimo
Sifa za mimea
·
Mimea imendwa na seli nyingi
·
Hujitengenezea chakula
·
Seli na ogani mpya hutengenezwa kwenye
ncha za mmea
·
Ina seli zenye ukuta wa seli
·
Hujilinda bila kujongea
·
Mimea ni eukarioti (seli zake zina
kiini)
·
Mimea haijisogezi toka sehemu moja
kwenda nyingine
·
Huhifadhi chakula kama wanga
Sifa za wanyama
·
Wanyama wameundwa kwa seli nyingi
·
Hawajitengenezei chakula
·
Seli zao hazina ukuta wa seli
·
Wanyama ni eukarioti
·
Wanyama hujisogeza sehemu moja kwenda
nyingine
·
Huzaliana kwa kujamiana
·
Huhifadhi chakula kama glykojeni
Tofauti
kati ya sifa za mimea na wanyama
Mimea
|
wanyama
|
Haina uwezo wa
kujisogeza
|
wana uwezo wa
kujisogeza
|
Hujitengenezea
chakula
|
Hawajitengenezei
chakula
|
Hutoa oksijeni nje na
kupokea kabondaioksaidi
|
Hupokea oksijeni na
kutoa kabondaioksaidi
|
Seli zao zina ukuta
wa seli
|
Seli zao hazina ukuta
wa seli
|
Huhifadhi chakula
kama wanga
|
Huhifadhi chakula
kama glykojeni
|
Mahitaji
muhimu kwa uhai na ukuaji wa wanyama na mimea.
1.mahitaji
muhimu kwa wanyama
a) Chakula
b) Hewa
c) Joto la wastani
d) Malazi
2.mahitaji
muhimu kwa mimea
a) Mwanga wa jua
b) Maji
c) Hewa
d) Joto la wastani
e) Madini
f) Virutubisho
No comments:
Post a Comment