Uhakiki
wa Fani katika riwaya ya Takadini
Hakiki fani katika riwaya ya Takadini
MWANDISHI: BEN J. HANSON
WACHAPISHAJI: MATHEWS BOOKSTORE AND STATIONARIES
MWAKA: 2004
JINA LA KITABU
Jina la kitabu TAKADINI lina maana ya “Sisi tumefanya nini”.
Hili ni jina ambalo Sekai alimpa mwanae mara baada ya kumzaa. Jina hili
lilitokana na majonzi aliyokuwa nayo juu ya kutaka kuuawa kwa mwanae na yeye
ilihali hawakuwa na hatia, ila tu kwa sababu ya mila za jamii yake zilivyotaka.
Jina hili la kitabu ni sadifu kwani linasawiri vyema maudhui yaliyomo katika
kitabu hiki. “Sisi tumefanya nini?’ ni swali ambalo linatokana na ukosefu wa
haki ya kuishi, kubaguliwa kutopendwa, na hata kutengwa kwa watu wenye matatizo
katika jamii. Swali hili linawalelekea wanajamii ambao bado wanashikilia mila
potofu zinazowakandamiza na kuwanyanyasa watu wenye matatizo mfano, ulemavu wa
ngozi, wagonjwa nk. Jina hili pia ni sadifu kwa maisha ya jamii yetu ya
watanzania kwani watu bado wanashikilia mila potofu ambazo si nzuri. Mwandishi
ametumia jina hili makusudi ili kutaka kuionesha jamii hali halisi ya vilio vya
albino, wasichana wadogo wanaolazimishwa kuolewa nk. Kuwa huu sasa ni muda
mwafaka wa jamii kuyaacha na kutupilia mbali mambo hayo.
MUUNDO
Muundo alioutumia mwandishi wa riwaya hii ni muundo wa msago au
kwa jina lingine muundo wa moja kwa moja. Ameyapanga matukio katika mtiririko
sahili kwani ameanza kutuonesha toka mwanzo mpaka mwisho wa maisha ya kijana
Takadini “Msope”.Toka kutungwa kwa mimba yake, kuzaliwa kwake na kuishi kwake,
matatizo na changamoto zinazomkumba na jinsi anavyokabiliana nazo na hatma ya
maisha yake.
Mgawanyo wa visa na mtukio umepangwa katika sura ambapo visa
vimejengwa kwa ufundi na kuvifanya vijengane na kukamilishana kuelekea kilele
cha masimulizi. Matukio haya yamewekwa katika sura kumi na tatu.
·
Sura ya
Kwanza:Sura hii inaanza kutuelezea kuhusu mwanamke
Sekai anavotunga mimba, pia tunaelezwa kuhusu mtazamo mbaya wa wake wenzie juu
ya mimba hiyo baada ya Sekai kukaa kwa muda mrefu bila ya kujaliwa mtoto.
·
Sura ya
Pili:Hapa tunasimuliwa jinsi Sekai anavyofanikiwa kujifungua salama.
Lakini kwa bahati mbaya kwa kawaida ya jamii yao anajifungua mtoto Zeruzeru
ambaye kwa mila zao mtoto huyo ni laana. Hivyo alipaswa kutupwa mara moja ama
kuuawa. Hakuna ambaye alikuwa tayari kumpokea mtoto yule kwani si baba yake
wala jamii yake ila mama yake pekee.
·
Sura ya
Tatu:Jamii bado haipo tayari kumpokea mtoto Sope, wanawake wenza wa
Sekai wanasubiri kwa hamu kuona tukio la kutupwa kwa Takadini litakavokuwa,
kwani ndio jinsi mila na taratibu za mababu zilivyotaka. Kutokana na hali hii
ndipo Sekai anapata wazo la kutoroka. Anaamua kuondoka kwenda mbali ili
kukinusuru kichanga kisicho na hatia kwani alisubiri kwa hamu na uchu wa muda
mrefu kupata mtoto.
·
Sura ya
Nne:Sekai anafanikiwa kutoroka na mwanae Takadini ili kumuepusha na
kifo, jamii na Mtemi wanapata habari ya kutoroka kwake. Upelelezi unafanyika
lakini juhudi hazikuzaa matunda kumpata Sekai na mwanae mchanga waliotakiwa
kuuawa. Sekai anasafiri mbali na kufikia kijiji kingine na kupokelewa na mzee
Chivero.
·
Sura ya
Tano:Sekai anapokelewa katika kijiji cha mzee Chivero, jamii na wazee
wanashitushwa sana na ujio huo lakini wanalazimika kumpokea tu baada ya malumbano
ya muda mrefu. Kwani mila ziliwataka kutowatelekeza wageni katika kijiji chao,
na hiyo ndiyo inakuwa mwanzo wa matumaini ya Sekai kuhusu kuishi kwa mwanae
ambaye alionekana kuwa ni laana ya mababu na hakupaswa kuishi.
·
Sura ya
sita:Baada ya Sekai kupokelewa katika kijiji cha mtemi Masasa, habari
za ujio wake zinaenea kwa wanakijiji wote na wanaonekana kushtushwa sana, si
hivo tu bali pia wanajiapiza katu kutomsogelea Sope kwani waliamini amelaaniwa.
Lakini kwa juhudi za mzee Chivero baba mpya mlezi wa Takadini Sekai anapata
rafiki. Tendai mke wa mtemi Masasa. Anajengewa kibanda cha kuishi yeye na
mwanae na maisha yanaanza.
·
Sura ya
saba:Sekai anaanza kujishughulisha na shughuli za kawaida kama mama
na mwanamke, analima bustani na kufanya kazi ndogo za nyumbani. Siku moja
katika safari ya kurudi nyumbani kwa bahati mbaya wanavamiwa na nyuki na
kujeruhiwa vibaya yeye na mwanae, anaamua kumtupia mwanae kichakani ili
kumuokoa na yeye kujitumbukiza mtoni. Wote wawili wanafanikiwa kutibiwa na
kupona majeraha.
·
Sura ya
nane:Taratibu Takadini anaanza kukua lakini anagundulika kuwa hawezi
kutembea vyema kwa mguu mmoja, hii ilitokana na kuvunjika Mguu baada ya
kurushwa kichakani na mamaye kama juhudi za kumwokoa. Hali hii inamhuzunisha
zaidi Sekai na Chivero kwani walimpenda sana. Hapa ndipo mapenzi ya Chivero
yalianza kudhihirika rasmi kwa Takadini kwani alijenga urafiki naye na kumpenda
kama mwanae. Alimfundisha utabibu wa dawa za kienyeji na mambo mengine mengi.
Pia tunaona watoto jinsi walivyombagua Takadini kutokana na hali yake, kwani
waliambiwa na wazazi wao wasicheze naye amelaaniwa hivo hawakuthubutu.
·
Sura ya
tisa:Katika sura hii, Mzee Masasi anafariki dunia na kumuacha mzee
Chivero katika majonzi makuu. Hali ya mzee Chivero nayo inaanza kuzorota kwa
uzee. Anampa Takadini usia mbalimbali na kumfunza. Pia tunaelezwa juu ya fikra
mpya za Takadini za kupiga “mbira” kifaa cha muziki cha kijadi, hii baada ya
kuvutiwa na sanaa hiyo aliposhiriki sherehe za mavuno za mwaka. Jamii bado
ilimtenga Takadini na kumbagua, walimwona si binadamu bali mzuka tu! Na kwa
bahati mbaya mzee Chivero naye aliaga dunia na kuacha simanzi kuu kwa Sekai na
Takadini mbao alikuwa ni tegemeo na faraja kwao.
·
Sura ya
kumi:Baada ya kifo cha mzee Chivero, Takadini anapata mwalimu maarufu
mpiga mbira mzee Kutukwa, anamfundisha kupiga mbira, Takadini anaonesha juhudi
kuu na kufanikiwa. Pia anmsaidia kifaa cha kumsaidia kutembea kutokana na mguu
wake mbovu, hii inakuwa ni faraja kubwa kwa Takadini na mamaye.
·
Sura ya
kumi na moja:Hapa tunaelezwa juu ya kijana
Nhamo adui mkuu wa Takadini kwani hakumpenda na alimdhihaki na kumdhalilisha
mara kwa mara. Kijana huyu anaonekana kuwa ni shujaa katika jamii yake kwa
kitendo cha kumuua simba mla mifugo. Hiyo inamletea sifa kubwa na majivuno
mengi hivo wasichana wengi kumtamani awaoe, hali ni tofauti kwa Shingai ambaye
anaonesha hisia za mapenzi kwa Takadini pamoja na hali yake ya “Usope”.
Chemchemi za mapenzi ya Takadini kwa Sekai zinaanza kumea jambo ambalo
linamkera sana Nhamo na kuzidisha chuki kwa Takadini kwani pia alitamani kuwa
na Shengai binti mrembo. Jamii inafanya kikao kujadili suala la Shengai
kumpenda Takadini na wanalipinga vikali suala hilo.
·
Sura ya
kumi na mbili:Nhamo anakata shauri na
kwenda kumposa Shengai, wazazi wa pande zote mbili wanaliunga suala hilo mkono
asilimia zote. Kwani hilo lingewanusuru aibu ya mwanao kuolewa na Sope, kwani
walijua fika Shingai alimpenda Takadini na hakumtaka Nhoma. Nhoma anamuonya
vikali Takadini kuwa asiendelee na lolote kwa Shengai. Pia hapa zinafanyika
sherehe ya kijadi ya kumkaribisha hayati mzee Chivero tena nyumbani.
·
Sura ya
kumi na Tatu:Wakati wa sherehe ya
mavuno, binti Shengai anashindwa kuvumilia na kuamua kumfuata Takadini
kibandani kwake. Anaamua kuvunja mila za kwao kwani alimpenda kwa dhati
Takadini, pamoja na dharau, kejeli, kubaguliwa, ulemavu wake na kuonekana kuwa
ni mtu aliyelaaniwa. Wazazi wake wanamtenga na kutomtambua kama ni mtoto wao
tena. Suala hilo linatikisa jamii ya watu wa kijiji kile na hata kutaka
kuwafukuza Sekai na mwanae lakini wanaokolewa na maamuzi ya busara ya wazee kwa
kuwacha Shengai na mpenziwe Takadini waishi hali wakisubiri matokeo! Kuwa je
mtoto atazaliwa sope? Na kuongeza ukoo wa masope na kijiji chao kuwa cha
masope? Hapa ndio inapojulikana hatma ya Takadini na mkewe kwani anapata
ujauzito na kufanikiwa kujifungua mtoto salama asiye Sope. Ilikuwa furaha kuu
kwa mama na mtoto na wote pia. Wanaamua kurudi kijijini kwao walikotoroka ili
kwenda kuwadhihirishia kuwa hata sope anaweza kuishi hapaswi kubaguliwa na
kutengwa
MTINDO
Mwandishi ametumia mitindo kadha wa kadha ili kuipamba kazi yake
na kuifanya ivutie wasomaji; mfano matumizi ya nafsi mbalimbali, matumizi ya
nyimbo nk.
Matumizi
ya nafsi
Kwa kiasi kikubwa yametawala matumizi ya nafsi ya tatu umoja na
wingi katika sura zote.Mfano.uk.
30. “ aliingia ndani na kuanza kazi.”Piauk.3 “ Sekai alikoka moto nje ya kibanda, akaketi na kuzungumza
na Pindai”.
Matumizi ya nafsi ya pili
au dayalojia
Mfano uk 29 - 30. Mazungumzo kati ya Chivero na Sekai:“je umelala salama?“je umelala salama?Sijambo mwanangu, sijui wewe?Sijambo Sekuru,Na
mwanao je?Naye hajambo.”
Matumizi ya nafsi ya
kwanza. Mfano uk. 82 na 83
“lakini ghafla nilipata nguvu mpya”;“nilikuwa na nguvu kama
kijana….”
Pia mwandishi ametumia nyimbo katika baadhi ya sura ili
kuwaburudisha na kuliwaza wasomaji. Mfano uk. 2 wimbo aliouimba mke mwenza wa
Sekai Rumbdzai.
“Mashamba yetu yamelimwa mbegu nazo zimepandwa zimechipua na
kumea, sisi watatu tumepanda mavuno yetu; mheshimiwa wetu amemiliki mavuno kwa
mikono yake halisi kutoka mashamba yetu yote lakini ni kipi alichoambulia
kutoka ardhi ile isiyomea kitu?”pia ametumia wimbo uk.
34, 57, 85.
Matumizi ya hadithi ndani ya hadithi pia ni mtindo mwingine wa
usimulizi alioutumia mwandishi.Mfanouk82Kutukwa alisimulia vijana
hadithi enzi ya ujana wake na jinsi alivopambana na maadui vitani.
Matumizi ya Lugha
Lugha aliyotumia mwandishi ni lugha fasaha na rahisi
inayoeleweka kwa wasomaji wake. Ametumia pia lugha nyinginezo kama vile lugha
za kikabila.Maneno kama vile“Amai”,lenye maana yamama,
“Sope”lenye maana yazeruzeru,
“shumba”- simba, “mbira” – chombo cha asili cha muziki, “gudza” – blanketi
lililotengenezwa kwa nyuzi za magome ya miti.nk.Hivyo mwandishi ametumia
lugha hii ili kuwaleta wasomaji kwenye mazingira halisi ya kiutamaduni ya jamii
ile.
Matumizi
ya tamathali za Semi
·
Tashibiha:Mfanouk. 6 “ muda huenda polepole mithili ya mwendo wa kakakuona
Uk.15 “ habari njema huchechemea kwa mguu mmoja lakina mbaya hukimbia kama
Sungura”Uk.16 “….. alibaki kama kinyago cha mpingo”.Uk.28 “ sio kufurika kama
Chura”Uk.33 “aligeuza shingo yake sawa na Mbuni”Uk.42 “ nywele kama vinyweleo
vya mahindi yaliyokaribia kukomaa”Uk.82 “muziki ulikuwa kama chemchemi ya maji
mwilini mwake”
·
Tashihisi:Mfanouk. 5 “ndege mbalimbali wakiimba kuikaribisha siku mpya”Uk. 7 “vivuli
vya jioni viliongezeka urefu”Uk. 18 “maneno yananila mifupa yangu”Uk 25 “kifo
kilinukia”
·
Tafsida:Mfano, uk. 83 “sehemu zake za siri”
·
Sitiari:Mfano,
uk. 88 “Tapfumaneyialigeukambogo” Uk.97“mwana Mbwa hakuiba mfupa”, Tawanda mfupa ulikwenda wenyewe kuchezanaye.” Hapa
mfupa umefananishwa na Shingai na Takadini ndio mwanambwa
Matumizi
ya Semi
·
Methali:Uk. 45 “ kipofu huwa hachagui shimo la kutegea wanyama”uk.33
“ moyo mwema utakufanya uuwawe”
·
Misemo:Mfano.Uk. 12 “kufikiri katika siri ni sawa na safari ya mbwa”Uk. 100
“kanga hawezi kutua juu ya bua la mtama”Uk.101 “kibuyu kikubwa hakikosi mbegu
ndani”Uk. 125 “fuvu la nyanilimekuwa kijiko kwa mlo wa mahindi”
·
Nahau:uk. 27 “ penzi langu kwake halikufua dafu”Uk. 88 “kutiana moyo
wa ari”
Matumizi
ya mbinu nyinginezo za kisanaa
·
Nidaa:Mfano,Uk.4 “Ha!” , “Ha! Atimuliwe tena? Mchawi?” Uk.16 “Mai,
Wee!” Uk.39. “Ha! Iwe! Ha!”
·
Mdokezo:MfanoUk.3 “ndiyo Pindai, ninaogopa……….” Uk.42 “mtu mzima kama
watu wenine ameamua………”
·
Takriri:Mfano,uk 57 “ mwanangu, mwanangu, mwanangu, wamekufanya nini?”
Wahusika
Sekai
·
Ni mke wa Makwati wa
kwanza.
·
Ni mwanamke jasiri.
·
Anapinga mila potofu na
mbaya za jamii yake.
·
Ni mvumilivu.
·
Ni mchapakazi mzuri.
·
Anajifungua mtoto
zeruzeru ambaye ni laana kwa jamii yake.
·
Ni mtiifu na mwenye adabu.
·
Ana huruma na
mnyenyekevu.
·
Ana mapenzi ya dhati.
·
Anafaaa kuigwa na jamii.
Takadini
·
Ni mtoto anayezaliwa na
ulemavu wa ngozi( albino)
·
Anasadikika kuwa ni laana
kwa jamii yake hivyo kupaswa kuuawa au kutupwa mbali.
·
Anaokolewa na mama yake
kwa kutoroshewa katika kijiji kingine.
·
Anapokua anakua kijana
jasiri.
·
Hapendwi na jamii.
·
Anabaguliwa na jamii,
hana rafiki.
·
Ni mvumilivu na msikivu
mwenye heshima.
·
Alimpenda Chivero sana.
·
Alikuwa mpiga mbira
(chombo cha muziki cha kijadi) maarufu.
·
Alimuoa Shingai na kupata
mtoto asiye Sope.
Makwati
·
Mume wa Sekai.
·
Ameoa ndoa ya mitara ana
wake wanne.
·
Anashikilia mila na
desturi potofu.
·
Hana mapenzi ya dhati kwa
mwanae.
·
Hafai kuigwa na jamii.
Dadirai na Rumbidzai
·
Wake wengine wa mzee
Makwati.
·
Wana wivu.
·
Hawampendi Sekai.
·
Wana roho mbaya kwani
wanamwombea Sekai mabaya.
·
Ni katili kwani
wanashinikiza Sekai na mwanae wauawe bila huruma.
·
Wasengenyaji.
·
Hawafai kuigwa na jamiii.
Pindai
·
Mke wa pili wa Makwati.
·
Ana upendo wa dhati kwa
Sekai.
·
Ni mkweli.
·
Hana wivu.
·
Ni mshauri mzuri.
·
Anafaa kuigwa na jamii.
Chivero
·
Ni mzee wa kijiji cha
mzee Masasa.
·
Anawapokea Sekai na
mwanae baada ya kutoroka kwao kwa ukarimu mkubwa.
·
Ni mwenye roho nzuri.
·
Ana huruma sana.
·
Ni mganga wa tiba za
asili.
·
Ana mapenzi ya dhati kwa
Takadini na Sekai.
·
Anamrithisha Takadini
uganga.
·
Ana busara na hekima.
·
Ni mshauri mkuu wa Mtemi
Masasa.
·
Anafaa kuigwa na jamii.
Mtemi Masasa
·
Ana busara na hekima.
·
Ana huruma.
·
Anafuata mila na desturi
ya jamii yake.
·
Ni msikivu.
·
Ni rafiki mkubwa wa
Chivero.
·
Ni kiongozi bora.
Nhamo
·
Ni kijana katika kijiji
cha mtemi Masasa.
·
Ana majivuno na jeuri.
·
Hampendi Takadini kwani
alimbagua kumpiga na hata kumdhalilisha.
·
Hafai kuigwa n ajamii.
Tendai
·
Mke mdogo wa mwisho wa
mtemi Masasa.
·
Aliolewa bila kupenda,
hakumpenda mtemi Masasa kwani alimzidi umri.
·
Alikuwa rafiki mzuri wa
Sekai.
·
Ana mapenzi ya dhati kwa
Takadini.
·
Ana bidii na mvumilivu.
Nhariswa na mkewe
·
Ni wazazi wa Shingai
·
Wanashikilia mila desturi
potofu
·
Hawakupenda kabisa
kitendo cha mtoto wao kumpenda Takadini
·
Walimlazimisha kuolewa na
Nhamo kwani walitaka sifa na maujiko
·
Walimtenga Shingai baada
ya kutoroka na kuolewa na Takadini
·
Si wazazi wazuri
·
Hawafai kuigwa na jamii
Kutukwa
·
Ni mzee katika kijiji cha
mtemi Masasa
·
Ni mpigaji mbira maarufu
·
Alimfundisha Takadini
kupiga mbira
·
Alitoa mtazamo mbaya kwa
wanakijiji wenzake kwa kuwaeleza sifa nzuri za Takadini
·
Alimpenda Takadini.
Anafaa kuigwa na jamii
Mandhari
Mandhari aliyotumia Ben J Hanson ni mandhari ya kijijini kwani
maisha ya watu na mazingira yanayoelezwa ni ya kijijini, masuala kama ya
kilimo, ufugaji, sherehe za mavuno, makazi ya watu kukaa katika jumuiya ya
pamoja kijamaa inayoongozwa na mtemi mmoja. Mfano mtemi Masasa, yote haya ni
viashiria kuwa mandhari ni ya kijini. Mandahari ambayo mwandishi ameijengea
mawazo yake na kuyaibua ni sadifu na halisi. Kwani maeneo ya vijijini ndiko
kulikokithiri mambo ya imani potofu na za kishirikina kama vile kuwaua watoto
Sope au albino.
No comments:
Post a Comment