Muundo
wa Insha
Katika uandishi wa insha, muundo wake unakuwa na vitu
vifuatavyo:
1.
Kichwa
cha insha; kichwa cha insha hudokeza kile ulichokijadili katika insha
yako. Kwa mfano: Madhara ya matumizi ya madawa ya kulevya n.k
2.
Utangulizi; Mambo
yaliyopo katika utangulizi ni pamoja na kutoa fasili ya maneno muhimu na
kuelezea kwa muhtasari mambo ambayo utakwenda kuyajadili katika insha yako.
3.
Kiini
cha insha; katika kiini ndipo kuna maelezo ya kina juu ya kile
unachokijadili katika insha yako, maelezo haya yanakuwa katika aya kadhaa
kulingana na idadi ya hoja ulizonazo katika mjadala wako.
4.
Hitimisho; hapa
ndipo kuna muhtasari wa kile kilichojadiliwa katika kiini cha insha au inaweza
kuwa ni msimamo juu ya kile kilichohadiliwa katika insha.
No comments:
Post a Comment