Fani katika
Ushairi wa Mashairi ya Chekacheka
Hakiki fani katika Ushairi wa Mashairi ya Chekacheka
MWANDISHI: THEOBALD A. MVUNGI
WACHAPISHAJI: EDUCATIONAL PUBLISHERS AND DISTRIBUTORS LTD.
MWAKA: 1995
MUUNDO
Mwandishi ametumia muundo wa tarbia, mashairi yake yote
yamefuata muundo huu. Beti za mashairi yake zina mistari minne. Mengi ya
mashairi yake, mistari imegawanyika katika vipande viwili yaani mistari ina
vina vya kati na vya mwisho. Mfano katika shairi la “Mashairi ya “Ngulu”;
Pia katika baadhi ya mashairi yake ameyaumba katika kipande
kimoja, yaani yana kina cha mwisho tu. Mfano ni mashairi kama vile ya“Dhahabu ya fahari”, “Utu umekuwa kima”,“Seng’enge”mfano katika shairi la“Utu umekuwa kima”
MTINDO
Mtindo aliotumia mwandishi ni mtindo wa kimapokeo kwani
amezingatia vigezo vya vina na mizani katika utunzi wa mashairi yake. Mfano
katika shairi la”“Tuambae ukasuku”
MATUMIZI YA LUGHA
·
Tashibiha:“Mshairi jihadhari, usishikwe kama fimbo.” – “Tuambae ukasuku.”“Na
wasiothaminiwa, wapimwao kama nyasi”- “Raia si mali kitu”“Mapenzi yasinadiwe,
kama shati dukani” – “Penzi lisilo heshima”“Utaliwa kama pumba” – “Utaliwa kama
pumba”“Kaburu si mtu hata, kwake sisi sawa punda” – “Utumwa huru”.“Pungufu
akili yake, mla punje kama kuku” – “Tuambaeukasuku”
·
Tashihisi:“Mejaribu kujongea, ndege awe mkononi,Yeye juu hurukia, namuomba
samahani.” – “Njiwa kiumbe mtini”“Moyo nimeshauri, lakini umekaidiMoyo kiburi
hatari, mfanowe kama radiMoyo mefumbata shari, unayakwepa marudi,Moyo u mwilini
mwangu, jirudi tuwe pamoja.” – “Moyo”Nipishe wewe senge’nge” –
“Seng’enge”.“Kijiji kisichoringa” – “Mashairi ya Ngulu”.“Akili yamsaliti,
kikongwe haoni kweli.”- “ Ni wapi ushauri?”
·
Sitiari:“Mshairi awe Nyati”- “Tuambae ukasuku”“Sisi ni miamba gogo”-
“Raia si mali kitu”“Ile chai kikombeni, rangi yake Mwafrika” – “Chai”.“Kwetu
ulikuwa mama” – “Indira”“Utu umekuwa kima” – “Utu umekuwa kima”“Uroho umekujaa,
watu mefanya kondoo” – “Utaliwa kama pumba”
Matumizi
ya semi
·
Misemo:“Fedha fedheha” – “Chanzo cha huo uozo”
·
Methali:“Akishaoza samaki, busara ni kumtupa” – “Chatu mmeza matonge”
·
Nahau:“Wabunge waote meno, wasivilambe viatu” –wawe na
mamlaka– “Tuambae ukasuku”Mbinu
nyingine za kisanaa
·
Takriri:“Chai ninaipa hati, kwa kutukidhia haja,Chai imewekwa kati,
kwetu sisi sote waja,Chai majani ya miti, hii miti yenye tija.” – “Chai”Neno“njiwa” limejirudia katika kila
ubeti –“Njiwa”Neno “moyo” limerudiwa katika kila
ubeti. – “Moyo”Neno “mauti” limejirudia katika
ubeti wa kwanza – “Utaliwakamapumba”Neno “Ngulu” katika mashairi ya “Ngulu”.
Ujenzi
wa Taswira
“Matonge”- madaraka-“Mwinyi
umewasha moto”“Nyati”– watawala –“Tuambae ukasuku”“Mfugaji”–
mwananchi – “Tuambae ukasuku”“Jiko”– madaraka “Kuna
nini huko jikoni”“Chatu”– watawala –“Chatu mmeza matonge”“Chura”– mtu
asiye na msimamo - “Chura
umegundulika”
No comments:
Post a Comment