Friday, November 29, 2019

HALI TATU ZA MAADA

HALI TATU ZA MAADA

Maada
Ni kitu chochote chenye uzito na kinachoshika nafasi.mf jiwe,kalamu,maji,mafuta nk.
Aina/namna/Hali za maada
1.      Yabisi
2.      Kimiminika
3.      Gesi
Yabisi ni hali ya maada ambayo ina msongamano mkubwa wa chembe chembe ndogo ndogo sana zinazounda maada.mf.jiwe,barafu,kiti,karatasi nk.
Sifa za maada yabisi
·         Ina msongamano mkubwa wa chembe chembe ndogo ndogo sana zinazounda maada (atomi)
·         Ina umbo maalumu
·         Ina ujazo maalumu
·         Molekyuli  haziko huru kutembea ila kutetemeka tu
·         Haiwezi kugandamizwa
Maada kimiminika
Ni hali ya maada yenye msongamano wa wastani wa chembe chembe ndogo ndogo sana zinazounda maada (atomi/molekyuli).mf. maji,mafuta ya taa,mafuta ya petrol,maziwa ya wanyama.nk.
Sifa za maada kimiminika
·         Ina msongamano wa wastani wa chembe chembe ndogo ndogo sana zinazounda maada
·         haina umbo maalumu,umbo lake hutegemea umbo la chombo kilichobeba maada
·         Ina ujazo maalumu
·         Molekyuli ziko huru wastani katika kutembea
·         Molekyuli zinaweza kugandamizwa kidogo sana
Maada ya gesi
Ni hali ya maada ambayo ina msongamano mdogo sana wa atomi/molekyuli.mfano gesi zote kama kabonidaioksaidi,oksijeni,haidrojeni,mvuke nk.
Sifa za maada gesi
·         Ina msongamano mdogo wa molekyuli/atomi
·         haina umbo maalumu
·         haina ujazo maalumu
·         Molekyuli ziko huru kutembea
·         Molekyuli  zinaweza kugandamizwa kwa kiasi kikubwa



Aina za mabadiliko katika maada
1.      Badiliko la kiumbo
2.      Badiliko la kikemikali
Badiliko la kiumbo: ni aina ya badiliko katika maada ambalo si la kudumu.mf kuungua kwa mshumaa,kuyeyuka kwa barafu.
Badiliko la kikemikali:ni aina ya badiliko katika maada ambalo ni la kudumu.mf.kuungua kwa karatasi,chuma kupata kutu,kuchacha kwa maziwa ,nk
Tafauti kati ya badiliko la kiumbo na la kudumu
Badiliko la kiumbo
Badiliko la kikemikali

I. sio la kudumu
II. Uzito wa kitu haubadiliki
III. Kitu kipya hakitokei
IV. Tabia ya kitu haibadiliki baada ya badiliko


I. Ni badiliko la kudumu
II. Uzito wa kitu hubadilika
III. Kitu kipya hutokea
IV. Tabia ya kitu hubadilika baada ya badiliko


No comments:

Post a Comment

CHUO CHA UALIMU MONTESSORI-MTWARA

Uhakiki Fani katika Ushairi wa Malenga Wapya

Fani katika Ushairi wa Malenga Wapya Hakiki Fani katika Ushairi wa Malenga Wapya MWANDISHI: TAASISI YA KISWAHILI, ZANZIBAR WACHAPISHA...