Fani
katika Riwaya ya Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe
Hakiki fani katika Riwaya ya Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe
JINA LA KITABU: NGOSWE PENZI KITOVU CHA UZEMBE
MWANDISHI: EDWIN SEMZABA
WACHAPISHAJI: NYAMBARI NYANGWINE PUBLISHERS
MWAKA:2006
UTANGULIZI WA KITABU
Ngoswe penzi kitovu cha uzembe ni tamthiliya maarufu sana ambayo
imewahi kuigizwa katika redio Tanzania na katika majukwaa mbalimbali hapa
nchini. Ni tamthiliya ambayo imeundwa vyema katika vipengele vya fani na
maudhui. Ameteua lugha nzuri na yenye mvuto kwa wasomaji yenye mbinu za
kifasihi zilizosheheni, muundo wenye mtiririko mzuri, unaoakisi kuanza
kuchipuka kwa matukio mpaka kilele cha matukio. Wahusika wamebeba vyema uhusika
wao mfano Ngoswe.
Ameibua dhamira kuhusu mambo yanayoigusa jamii ya leo kama vile
uzembe, madhara ya ulevi, uzembe kazini, suala la matabaka kati ya mjini na
vijijini. Mtazamo, falsafa na msimamo wake ni kulenga kuibadilisha jamii na
kuleta maendeleo.
JINA LA KITABU
Jina la kitabu “Ngoswe penzi kitovu cha uzembe” ni jina ambalo
limesawiri vyema yaliyomo ndani ya kitabu hicho, kwani Ngoswe ndio jina la
mhusika mkuu anayebeba dhamira kuu ya tamthiliya. Pia penzi limeonekana kuwa ni
kitovu cha uzembe kwani ndio yaliyopelekea kuteketezwa kwa karatasi za takwimu
za sensa. Hivyo jina la kitabu si tu kwamba limesawiri yaliyomo katika kitabu
bali pia katika jamii.
MTINDO
Mtindo alioutumia mwandishi ni dayalojia au majibizano.
Mwandishi amepanga visa na masimulizi kwa kutumia majibizano ya wahusika.
·
Matumizi
ya nafsi ya kwanza. Mwandishi ndiye
ameyafafanua na kuelezea baadhi ya matukio. Katika karibu kurasa zote mwandishi
ameonekana kuwa ndiye msimuliaji wa matukio.
·
Matumizi
ya nafsi ya pili. Hapa watu wawili na
zaidi wanajibizana. Tamthilya hii wahusika wanaojibizana kuibua dhamira na
migogoro. Kuna majibizano baina ya mzee Mitomingi, Ngoswe na Mazoea nk.unaweza
kupata mfano uk. wowote kwani ndio mtindo uliotawala.
MUUNDO
Muundo uliotumika ni muundo wa mojakwamoja au sahili. Kwani
ameonesha tangu mwanzo wa mambo mpaka mwisho, anajenga visa vidogo mpaka visa
vikuu au kileleni.Amepanga visa na matukio yake katika maonesho matano. Kila
kichwa kina maelezo yaliyojadiliwa katika onesho hilo.
·
KIJITO:Hapa
yanaeleza jinsi mambo yanavyoanza. Jinsi Ngoswe anavyoingia kijijini
anavyopokelewa na kuanza kufahamiana na wenyeji wake.
·
VIJITO:Hapa
Ngoswe anaanza kufanya kazi iliyompeleka kijijini na tunaanza kuoneshwa
changamoto anazokumbana nazo.
·
MTO:Ni
mwendelezo wa matukio ya mwanzo hapa visa vinazidi kukua.
·
JITO:Hapa
Ngoswe anakumbana na changamoto nyingi zaidi katika kazi yake. Na hapa anazidi
kuanguka kwani anajiingiza katika mapenzi na msichana Mazoea, anaendekeza ulevi
na kuharibu kazi kabisa.
·
BAHARINI:Hapa
inaoneshwa mwisho wa mambo jinsi yalivyokuwa. Yanaonekana mahojiano baina ya
Serikali na Ngoswe na Mitomingi juu ya uzembe uliofanyika wa kupoteza takwimu
na hapa ndipo suluhisho linapotolewa juu ya matatizo hayo.
WAHUSIKA
NGOSWE
·
Kijana wa kiume umri kati
yamiaka 20-25
·
Ameelimika na
amestaarabika
·
Anatumwa na serikali
kufanya sensa kijijini
·
Anajihusisha na mapenzi
na msichana mazoea
·
Ni mlevi
·
Hana umakini katika kazi
·
Aliharibu kazi ya
serikali
·
Hafai kuigwa na jamii
MAZOEA
·
Ni msichana mwenye umri
kati ya miaka 18-20
·
Ni binti wa Mzee
Ngengemkeni Mitomingi
·
Hana elimu na
hajastaarabika
·
Ana nidhamu ya woga
·
Ana tama
·
Hana msimamo alikubali
kuchukuliwa na Ngoswe hali akijua alishatolewa mahari
·
Hafai kuigwa na jamii.
NGENGEMKENI MITOMINGI
·
Ni balozi katika kijiji
chake
·
Ni baba mzazi wa Mazoea
·
Ameoa ndoa ya mitara, ana
wake wawili
·
Hajaelimika
·
Anashikilia mila na
desturi za kale
·
Mlevi
·
Mkali sana
·
Anateketeza karatasi za
takwimu
MZEE JIMBI
·
Mwanakijiji
·
Hajaelimika kwani hajui
hata umri wake
·
Ni mlevi
·
Ana wake wawili
·
Anashikilia ukale
MAMA MAZOEA
·
Mke mkubwa wa Mitomingi
·
Mama yake Mazoea
·
Mlezi wa familia
·
Hapewi nafasi ya kutoa
maamuzi katika familia
MAMA INDA
·
Mke wa pili Mzee
Mitomingi
·
Mama yake Huzuni
·
Hapewi nafasi ya kutoa
maamuzi
·
Ni mlezi wa familia.
MANDHARI
Mandhari ya tamthiliya hii imechorwa katika mazingira ya
kijijini. Mambo yanayoelezwa ni ya kijijini mfano kilimo, hali ya watu
kimaisha, huduma duni sana za kijamii kama vile shule, umbali wa makazi toka
nyumba moja hadi nyingine. Haya yanatudhihirishia vyema mandhari hiyo ambayo
kwayo imeibua dhamira mbalimbali kama vile umaskini, ukosefu wa elimu, huduma
duni za afya vijijini, masuala ya imani potofu nk.
MATUMIZI YA LUGHA
Lugha aliyotumia mwandishi ni lugha fasaha na rahisi kueleweka
kwa wasomaji. Pia kuna matumizi ya lugha nyingine mfanouk. 1 “bell bottom”
Matumizi ya semi
·
Methali:Uk.22 “Penye nia pana njia”.Uk.27 “Waona vyaelea vyaundwa.”
·
Misemo:Uk.14 “Akuwaniae ujovu haji kweupe”
·
Nahau:Uk.11 “hebu keti tutupe mawe pangoni” –tule
chakulaUk.7 “mbongo zimelala”-ana
maarifaUk.14 “pombe na yeye ni
pete na chanda”- anapenda pombe sana.
Matumizi ya tamathali za
semi
·
Tafsida:Uk.21 “Wala hajarudi, kama ingekuwa ni kujisaidia si angekuwa
amekwishamaliza?”
·
Tashbiha:Uk.1 “vumbi jekundu kama ugoro wa subiana”Uk.8 “sarawili yake
miguuni kama kengele ya bomani”Uk.17 “wanaondoka huku wakitazamwa kama vile
mizuka”
·
Sitiari:Uk.7 Mama Mazoea : “kiziwi mkubwa wee!”Uk.14 “pombe na yeye ni
pete na chanda!”Uk.26. “karatasi? za takwimu? Ndio wanyama gani hao?”
·
Mubaalagha:Uk.11 Mama Mazoea : “kupeleka chakula ndio umefanya makao!”Mama
mazoea : “Kujibu swali ndio ukachukua mwaka mzima!”
Mbinu nyingine za kisanaa
·
Mdokezo:Uk.22 Mazoea : “sijui….. siwezi….. namuogopa baba”Uk.16 Ngoswe :
“huyo mtoto wenu wa kwanza anaishi hapa au…..”
·
Takriri:Uk.9 “Mama Masikio! We Mama Masikio!”Uk.13. “Hodi! Hodi!”Uk.2
“karibu karibu”
·
Tashtiti:Uk.5 Ngoswe: “hivyo waitwa nani?”Mazoea: “mie?”Uk.22 Ngoswe:
“mchumba? Kwani mchumba ni kitu gani?”Uk.26 Mitomingi: “karatasi? Za takwimu?
Ndio wanyama gani hao?Hapa wahusika waliuliza
maswali ambayo majibu yake waliyaelewa ila kutokana na kutaka kudhihirisha
hasira, msisitizo nk. Ndio maana wametumia tashtiti.
·
Onomatopea/tanakali
sauti:Uk.7 Kifaruhande anacheka
“Ha! ha! ha!
Ujenzi wa taswira
Mwandishi ametumia taswira ya mto kuelezea visa vyake. Sehemu ya
kwanza ni sehemu ya kijito, kijito ni kimto kidigo mwandishi hapa anaanza
kueleza mambo yakiwa machanga kabisa ndio yanaanza.
Sehemu ya pili ni vijito. Huu ni muunganiko wa vijito
vidogovidogo hapa mwandishi anaanza kueleza visa vidogovidogo. Sehemu
inayofuata ni sehemu ya Mto. Hii inaashiria mambo yameanza kuwa mazito, visa
vinakua zaidi na Ngoswe anazidi kuingia katika changamoto kubwa zaidi.
Pia Jito ni taswira ambayo mwandishi ameitumia kuashiria hatari
zaidi mambo makubwa zaidi na hapa ndipo tunaona Ngoswe anaanguka kabisa katika
kazi yake kwani Jito ni lenye maji mengi na yanayoenda kwa kasi hivyo huhitaji
umakini mkubwa zaidi.
Mwisho sehemu ya Bahari ambapo hapa ndipo hatima ya mambo
inaelezwa Ngoswe anazama na kupotea kabisa! Hafanikiwi kutoa takwimu kwani
karatasi zilichomwa moto.
No comments:
Post a Comment