Fani
katika Tamthiliya ya Kilio Chetu
Hakiki fani katika tamthiliya ya Kilio Chetu
MWANDISHI: MEDICAL AID FOUNDATION
WACHAPISHAJI: TANZANIA PUBLISHING HOUSE (TPH)
MWAKA: 1996
JINA LA KITABU
KILIO CHETU ni jina ambalo linaasadifu yaliyomo katika kitabu.
Masuala yanayotajwa mule kama vile upotofu wa maadili kwa vijana wadogo kama
Suzi na Joti, suala la mimba za utotoni, madhara ya gonjwa hatari la UKIMWI kwa
jamii kweli ni kilio chetu ni kilio cha Taifa zima. Kwani katika mambo
yanayoiyumbisha jamii kimaendeleo ni upotovu wa maaadili.
Jina hili ni sadifu katika jamii. Mwandishi amelitumia wakati
muafaka kabisa kwani mambo anayoyaeleza ndio changamoto katika jamii ya leo.
Hivyo kupitia hili jamii si budi kubadilika.
UTANGULIZI WA KITABU
Kilio chetu ni tamthiliya ambayo imejieleza vyema katika fani na
maudhui. Tamthiliya hii inamuhusu mhusika Suzi na Joti ambao ni watoto wadogo
sana. Wanajiingiza katika mapenzi katika umri mdogo kutokana na ukosefu wa
elimu ya kijinsia. Inatueleza kuhusu athari za ugonjwa huu usiobagua. Pia
tunafahamishwa kuhusu mtazamo wa wazazi na walezi kuhusu utoaji wa elimu ya
jinsia kwa vijana wao. Wapo wanaolipokea kwa mtazamo chanya na wengine hasi.
Kwa ujumla ni tamthiliya nzuri kwani ina mtazamo wa kimabadiliko
unaolenga kuwakomboa vijana wetu kutoka katika janga la ugonjwa hatari wa
UKIMWI.
MUUNDO
·
Sehemu
ya kwanza:Inaonesha jinsi gonjwa la UKIMWI linavyoikumba
jamii. Mwandishi anaeleza kuhusu Dubwana linaloikumba jamii.
·
Sehemu
ya pili:Mwandishi anaeleza kuhusu athari za UKIMWI,
jambo ambalo lilipelekea kifo cha Fausta. Pia Suzi agundulika kujihusisha na
mapenzi baada ya kukutwa na vidonge vya kuzuia mimba.
·
Sehemu
ya tatu:Inaeleza juu ya watoto ambao wameshajiingiza
katika suala la mapenzi licha ya kuwa na umri mdogo mfano ni Joti na Suzi. Pia
madhara ya utandawazi yanaelezwa hapa mfano kuoneshwa kwa picha za ngono.
·
Sehemu
ya nne:Tunaelezwa juu ya tabia hatarishi za Joti za
kuwa na mahusiano na wasichana wengi mfano Chausiku, Yoranda, Gelda na Suzi.
Hapa Joti anafanikiwa kumrubuni tena Suzi. Pia tunaoneshwa jinsi Ana
anavopingana na vishawishi kutokana na kupata elimu ya jinsia.
·
Sehemu
ya tano:Suzi anagundulika kuwa na mimba ya Joti,
anajutia kosa hilo anajilaumu sana.
·
Sehemu
ya sita:Inatuonesha jinsi Joti alivyokuwa magonjwa
tayari kutokana na UKIMWI. Hapa ushauri mzuri unatolewa kuhusu namna ya
kumtunza mgonjwa wa UKIMWI na kumfanya aishi kwa matumaini. Hapa mwandishi
anapinga mila potofu kuhusu UKIMWI kuwa si kurogwa bali ni ugonjwa
unaoambukizwa.
MTINDO
Tamthiliya hii imesheheni katika mitindo kadha wa kadha
inayopamba kazi hii. Mtindo uliotumika ni dayalojia au majibizano.
Mwandishi ametumia mtindo wa mianzo na miisho ya kifomula ya
usimulizi ambao ni mtindo wa usimulizi wa fasihi ya kiafrika. Mfanouk.1 mwandishi anasema “paukwa….. pakawaa…. Niendelee….
nisiendelee? ….. au mmechoka? Uk.113,piauk.36 mwandishi anasema “na hadithi yangu imeishia hapo”.Pia mwandishi ametumia mtindo wa utambaji kwani ndiye
anayesimulia na kuelezea matukio.
Matumizi
ya nafsi
Nafsi ya pili ndiyo iliyotawala, mwandishi ametumia majibizano
ya watu wawili mfano Suzi na Joti, pia watu watatu n.k.Pia mwandishi ametumia
tanzu nyingine za fasihi mfano wimbo uk.27
Wahusika
SUZI
·
Ni binti mdogo wa darasa
la sita
·
Anajihusisha na mapenzi
na Joti
·
Hana msimamo
·
Anapata mimba katika umri
mdogo
·
Ana hatari ya kuwa na
UKIMWI
·
Hakupewa elimu ya jinsia
·
Ana tamaa kwani alitamani
vitu alivyohongwa na Joti.
JOTI
·
Ni kijana mdogo wa kiume
·
Ana mahusianao ya mapenzi
na wasichana wengi Suzi, Gelda, Yoranda na Chausiku
·
Hana elimu ya jinsia
·
Ana makundi mabaya ya
marafiki
·
Anaathirika na kufa kwa
gonjwa la UKIMWI
·
Amechangia kuharibu
maisha ya Suzi kwa kumrubuni
·
Ni mlaghai
·
Hafai kuigwa na jamii
MAMA SUZI
·
Ni mzazi wa Suzi
·
Anashikilia ukale hataki
mabadiliko
·
Hampi mwanae elimu ya
jinsia
·
Alichangia kuharibu
maisha ya Suzi
·
Ni mkali sana katika
malezi hatumii busara bali hasira
·
Hafai kuigwa na jamii
BABA JOTI
·
Ni mzazi wa Joti
·
Hayupo tayari kutoa
elimua ya jinsia
·
Anashikilia ukale
·
Ni mkali anatumia viboko
kuelimisha jambo ambalo si sahihi
·
Amechangia kuharibu
maisha ya Joti
·
Ni muhuni, si muaminifu
katika ndoa yake
·
Hafai kuigwa na jamii
ANNA
·
Ni binti mdogo wa shule
·
Ana elimu ya jinsia
·
Ana msimamo mzuri
anashinda vishawishi
·
Anatoa elimu kwa vijana
wenzake kuhusu athari za kujiingiza katika mapenzi katika umri mdogo
·
Ana tabia njema
·
Hana tama
·
Anafaa kuigwa na jamii.
BABA ANNA
·
Ni mzazi wa Anna
·
Anatoa elimu ya jinsia
kwa wazazi na watoto
·
Ni mlezi bora
·
Alichangia maisha ya Anna
kuwa ya mafanikio
·
Anafaa kuigwa na jamii
MJOMBA
·
Ni kaka yake Mama Suzi
·
Anaendana na wakati wa
sasa
·
Anatoa elimu ya jinsia
kwa vijana na wazazi
·
Ni mlezi bora ni mshauri
bora
·
Anatoa elimu ya UKIMWI
kwa Baba Joti anapinga mila potofu
·
Anafaa kuigwa na jamii
MAMA JOTI
·
Mzazi wa Joti
·
Ndoa yake ipo matatani
kuingiliwa na mke mwingine
·
Anaelewa kuwa jamii
imebadilika na wazazi wanapaswa kuwaelimisha watoto
JIRANI
·
Ni jirani wa Baba Joti
·
Ana imani potofu za
kishirikina, anaamini Joti alilogwa
·
Haamini kuwa UKIMWI upo
CHAUSIKU
·
Ni msichana wa mtaani
·
Mfanyabiashara wa
vitumbua
·
Ni jirani wa Suzi
·
Ana tabia mbaya ni muhuni
·
Alichangia kuharibu
maisha ya Joti
·
Ana mahusiano ya kimpenzi
na vijana wadogo mfano Joti na watu wazima pia, mfano Mpemba.
CHOGO,
MWARAMI NA JUMBE
·
Ni marafiki wa Joti
·
Ni wanafunzi wadogo
·
Si marafiki wazuri
·
Wana tabia mbaya
wanashauriana kuhusu mambo mabaya
·
Hawafai kuigwa na jamii
MANDHARI
Mandhari aliyoitumia mwandishi ni ya mjini, hii ni kutokana na
maelezo ya mhusika jirani anaposemauk.32 “……mie toka siku ile nimwone hospitali sijakaa mjini.
Nilikwenda zangu shamba kupambana na Nyani wala nafaka.”Pia lugha ya mtaani iliyotumiwa na vijana Joti, Mwarami na
wenzake, masuala ya picha ya “X” yaani viashiria vya mambo ya mjini kwani
yamekithiri sana mijini. Maeneo yanayotajwa kama vile uwanja wa Sabasaba ni
uwanja uliopo mjini, masuala ya lifti kwa wasichana hasa wanafunzi yapo mijini.
Mfano.uk.27 pia kuna mandhari ya nyumbani na mtaani.
Mandhari aliyotumia mwandishi inasawiri maudhui yake katika
jamii. Kwani anaibua mambo yaliyo katika jamii.
MATUMZI YA LUGHA
Lugha iliyotumika ni lugha iliyo na ubunifu wa kipekee wenye
mvuto wa kisanaa. Lugha ni rahisi na inayoeleweka vyema kwa hadhira lengwa. Pia
kuna matumizi ya lugha nyingine mfano kiingereza na lugha za kikabila. Kiingereza
mfanouk.21 “tuition” uk.16
“come”.Lugha za kikabila mfano wimbo uk.35“Joti afitwe sanda salauya; Ena ena salauya …………………….”
Matumizi ya lugha ya
mtaani
Mfanouk.16
“mshefa” “mshikaji”-rafiki.Uk.17 “kamba” –kudanganya jambo;Uk.22 “vidosho” –wasichana;Uk.16 “kanitolea nje”–
kukataa jambo fulani.
Matumizi ya tamathali za
semi
·
Tashibiha:Uk.1 “wakapukutika kama majani”Uk.5 “mgumu kama mpingo”Uk.6
“miti inaungua kama mabua”Uk.13 “Dubwana limetanda kama utando wa Buibui”
·
Tashihisi:Uk.2 “vifo vikawazoa”kifo huua
tu lakini kimepewa uwezo wa kuzoa
·
Sitiari:Uk.8 “We Mbwa mweusi”Uk.9 “Nyoka wee”Uk.21 “huyo kinyago wako
anakimbia nini?”
·
Tafsida:Uk.4 “kafa kwa kukanyaga nyaya”– kafa
kwa UKIMWI
·
Mubaalagha:Uk.4 “Mtu si mtu, kizuka si kizuka”
Matumizi ya mbinu
nyingine za kisanaa
·
Tanakali
sauti/ Onomatopea:Uk. Joti akasema“….acha moyo unipwite “Pwi! Pwi! Pwi!”Uk.25 “….hebu nitolee
uchafu wako mie ptuu!”
·
Tashtiti:Uk.15 “….huyu ni Suzi kweli au nani?”Uk.36 “kwanini Joti………
kwanini Joti afe?”
·
Takriri:Uk.1 “watu wakapukutika, wakapukutika…..” “tunakwisha,
tunakwisha”Uk.2 “vifo vikawzoa, vikawazoa .…. vikawazoa”Uk.16 “piga domo, piga
domo”
Matumizi ya semi
·
Methali:Uk.6 “wembamba wa Reli Treni inapita”Uk.11 “mzazi usipomfunza
walimwengu watamfundisha”Uk.19 “shukrani ya Punda ni mateke”Uk.24 ‘Ndege mjanja
ananaswa na tundu bovu”
·
Nahau:Uk.6 “nimekuvulia kofia”-nakuheshimuUk.21 “anajigongagonga” –anajipendekeza
·
Misemo:Uk.4 “kuwa nyumanyuma kama koti”Uk.6 “kifua simkingii maana siwi
naye”Uk.7 “makapera kibao Mume wangu wa nini?”Uk.22 “mapenzi ni tiba”Uk.26
“…..unakimbilia suti na nepi hujavaa”
Matumizi ya taswira
uk.1 “dubwana” –ugonjwa wa UKIMWI;Uk.7 “Nguru” –aina ya Samaki wabaya–amefananishwa na mtu
mbaya;Uk.21 “kinyago”- Suzi.
No comments:
Post a Comment