HUDUMA
YA KWANZA
Huduma ya kwanza nimsaada wa haraka anaopewa mtu
aliyepata ajali au kuugua ghafla kabla ya kumpeleka hospitali.ni msaada
anaopewa mgonjwa kabla ya kumwona daktari.mfano huduma ya kwanza kwa mtu
aliyeungua na moto,huduma ya kwanza kwa mtu aliyeumwa na nyoka,huduma ya kwanza
kwa mtu aliyekunywa sumu.lengo kuu la huduma ya kwanza ni kuokoa maisha ya
mgonjwa.
Vifaa/vitu ndani ya
kisanduku cha huduma ya kwanza
Kifaa/kitu
|
Kazi katika
huduma ya kwanza
|
mkasi
|
Kukatia
vitu kama kamba,kitambaa,pamba nk
|
pamba
|
Kuasafishia
jeraha
Kufungia
jeraha
|
Mipira
ya mkononi
|
Kujikinga
dhidi ya maabukizi kupitia uwazi wa majeraha kwenye mikono
|
dawa
|
Kutuliza
maumivu.mf panado
Kuua
bacteria kwenye jeraha
|
Maji
safi na salama
|
Kusafishianjeraha
Kusafishia
vifaa
|
plasta
|
Kufunika
kidonda kidogo
|
bendeji
|
Kufunga
jeraha kwa kuzungusha
|
wembe
|
Kukatia
vitu
|
HUDUMA ZA KWANZA MBALIMBALI
Aina ya
Huduma ya kwnza
|
|
1.Aliyeumwa na nyoka na wadudu wenye
sumu kali.
Wadudu
wenye sumu kali ni kama nge,nyigu,
nyuki n.k
|
Dalili
za mtu aliyeumwa na nyoka/mdudu mwenye sumu kali
I.
Kuonekana kwa Jeraha sehemu aliyoumwa
II.
Uvimbe sehemu aliyoumwa
III.
Kuhisi maumivu makali ya jeraha
IV.
Mwili kupatwa ganzi
V.
Kuishiwa nguvu
hatua
a. Hakikisha
mgonjwa ametulia,asihangaike wala kutembea tembea
b. Mlaze
chali na asiinue sehemu iliyong’atwa juu zaidi ya usawa wa moyo
c. Ondoa
vitu vilivyombana kama pete au nguo
d. Funga
kamba juu ya jeraha
e. Muwahishe
kituo cha afya
f.
Kama nyoka/mdudu aliyemng’ata yupo (amekufa)
nenda naye kituo cha afya
Tahadhari
Ø Usioshe
sehemu iliyoumwa na nyoka/mdudu mwenye sumu kali
Ø Usikate
wala kunyonya sehemu iliyoumwa na nyoka/mdudu mwenye sumu kali
Ø Usijaribu
kumshika nyoka/mdudu mwenye sumu kali aliye hai
|
2.aliyezirai
|
Dalili za mtu aliyezirai
I.
Kutokwa na jasho
II.
Kutoweza kuitikia unachomuuliza
III.
Kupotea uwezo wa kuona
IV.
Mapigo ya moyo kwenda taratibu
V.
Kutoweza kuinuka mahali alipo
VI.
Kupumua kwa shida
Visababishi vya mtu kuzirai
·
Mshituko wa ghafla
·
Magonjwa
·
Ajali
Hatua
a. Mlaze
mgonjwa chali
b. Muangalie
mgonjwa kama anapumua
c. Nyanyua
miguu yake juu kama sentimita 30
d. Ondoa
vitu vilivyombana
e. Weka
kitambaa kibichi kwenye paji la uso wake
f.
Muwaishe kituo cha afya
|
3.Aliyeungua na moto
|
Hatua
a. Tumia
maji barid ya bomba kupooza jeraha
b. Safisha
na kausha jeraha
c. Funika
majeraha kwa bendeji au kitambaa safi
d. Muwaishe
kitua cha afya
|
4.alievunjika
mfupa (mguu au mkono)
|
Vifaa
Kipande cha barafu,miti(mbao) mbili,kamba
mbili na dawa za kupunguza maumivu
Hatua za
kufuata
a.
Ondoa nguo sehemu ya jeraha ibaki wazi
b.
Weka barafu
c.
Funga mbao mbili(miti) zilizonyooka upande
wa kulia na kushoto mwa mkono au mguu uliovunjika
d.
Muwaishe kituo cha afya
|
5.mtu
aliezama majini
|
Mazingira
hatarishi ya kusababisha kuzama majini
·
Kucheza kwenye mito mirefu,visima na
madimbwi
·
Shughuli za uvuvi
·
Kuvuka mito mikubwa kwa miguu
·
Kuogelea kwenye kina kirefu
·
Kuogelea wakati wa mvua
·
Kuchota maji bila uangalifu kwenye visima
virefu
Hatua za
kufuata/kutoa huduma ya kwanza
a.
Hakikisha unajua kuogelea na mtoe ndani ya
maji haraka sana
b.
Mlaze chali na msaidie kupumua kwa
kumbonyeza tumbo kwa uangalifu na kuachia
c.
Gandamiza tumbo taratibu na mwinue atapike
maji yaliyo katika mapafu
d.
Mpeleke muhusika hospitalini
|
6.mtu aliekunywa sumu
|
Tahadhari
ya uhifadhi wa sumu na bidhaa za sumu
·
Sumu/Bidhaa ya sumu iwe katika kifuko/chupa
yake husika yenye kibandiko.
·
Sumu/Bidhaa ya sumu iwekwe kwenye kabati
droo za juu na zifungwe kabisa
·
Sumu/Bidhaa ya sumu irudishwe sehemu husika
baada ya matumizi
·
Vyombo vilivyotumiwa na Sumu/Bidhaa ya sumu
visafishwe kwa maji mengi sa sabuni
·
Chupa na vifuko vyenye Sumu/Bidhaa ya sumu
vilivyotumika vichomwe haraka.
Hatua
za kufuata / kutoa huduma ya kwanza
a.
Kama mgonjwa anajitambua muulize sumu gani
amekunywa na mda gani kwa taratibu
b.
Mnyweshe maziwa mabichi kama yatapatikana
haraka
c.
Kama mgonjwa hajitambui angalia kama
anapumua
d.
Kama aina ya sumu ipo karibu basi soma
kibandiko au ichukue.
e.
Muwaishe kituo cha afya.
|
No comments:
Post a Comment