SELIMUNDU/ANEMIA
SELIMUNDU
·
Ni ugonjwa wa kurithi usioambukiza ambao seli
nyekundu za damu huwa na umbo la mwezi mchanga au mundu.
Mgonjwa wa selimundu damu yake huwa na seli nyekundu za damu
za duara na kiwango kikubwa cha seli nyekundu zenye umbo la mwezi
mchanga(selimundu)
Selimundu hazina uwezo wa kubeba hewa oksijeni inayotumika
mwilini
Dalili za anemia
selimundu
·
Kuchoka sana na kuwa dhaifu
·
Kupatwa na kizunguzungu
·
Kupatwa na maumivu ya kichwa
·
Kupatwa na baridi kwenye viganja vya mikono na
miguu
·
Rangi ya macho kuwa manjano
·
Maumivu mwili mzima
Tiba
·
Kubadilisha uboho (rojorojo inayojaza nafasi za katikati
za mifupa) kutoka kwa mtu asiye na ugonjwa
·
Tiba hii ni hatari sana maana kuna hatari ya
kupoteza maisha
·
Tiba nyingine ni kuongezwa damu,kupunguza
maumivu na kutumia antibiotiki
No comments:
Post a Comment