Fani
katika Tamthiliya ya Watoto wa Mama N’tiliye
Hakaiki fani katika tamthiliya ya Watoto wa Mama N’tiliye
MWANDISHI: EMMANUEL MBOGO
WACHAPISHAJI: HEKO PUBLISHERS
MWAKA: 2002
JINA LA KITABU
Jina la kitabu WATOTO WA MAMA NTILIE limesadifu yaliyomo ndani
ya kitabu, kinaeleza kuhusu maisha ya watoto wa mama ntilie. Maisha ya dhiki,
umaskini uliokithiri, maisha yasiyo ya faraja yaliyokosa malezi bora, chakula
bora, elimu, huduma ya afya nk. Jina la kitabu linaakisi yaliyomo ndani ya
kitabu na katika jamii yetu ya leo kwani akina mama wengi hawana kazi nzuri za
kuwaingizia kipato kikubwa na bado wanategemewa katika malezi. Mwandishi
ametumia jina hili ili kibua kero na matatizo yaliyoko katika jamii.
UTANGULIZI WA KITABU
Riwaya ya Watoto wa Mama N’tilie ni riwaya ambayo inasadifu
maisha ya Mtanzania wa leo. Inaangazia suala la umaskini na hali ngumu ya
maisha, wimbi la watoto wa mitaani, masuala ya uhalifu wizi na ujambazi, malezi
nk. Mwandishi Mbogo amejitahidi sana. Pia katika fani ametumia muundo na mtindo
wenye kuwavutia wasomaji pia kawaumba wahusika wake kwa usadifu wa hali ya juu
huku mandhari yake ikiwa ni halisi inayosawiri maisha ya Tanzania.
MUUNDO
Muundo uliotawala katika riwaya hii ni muundo wa rukia au rejea.
Mfano sura ya tatu mwandishi anatuelezea juu ya safari ya Mama ntilie kwenda
matombo uk.34. Lakini anaacha kisa hicho ndani ya sura hiyohiyo anaanza
kutuelezea juu ya kuzaliwa kwa watoto Kurwa na Doto na asili yao. Pia uk.80
mwandishi anatudokeza juu ya safari ya kwenda kwa Musa na hatuoneshi hatma ya
safari yake bali anarukia kisa kingine na kuanza kutuelezea juu ya Zita
kupandwa na kichaa uk.81. Vilevile uk.85-86 anatusimulia juu ya safari ya Mama
Zita na Zenabu kuelekea hospitali kumwona Zita lakini hatuoneshi hatma ya
safari yao bali anarukia kisa kingine na kuturudisha nyumbani kwa Mzee Lomolomo
na jinsi anavyofakamia pombe alafu anaturudisha tena kutuambia juu ya kifo cha Zita
hospitalini Muhimbili.
Mwandishi amegawa visa na matukio katika sura tano. Sura hizi
zimejengwa katika muundo unaotegemeana ili kukamilisha kilele cha masimulizi.
MTINDO
Mtindo aliotumia mwandishi ni wa masimulizi ya mjazo au lugha ya
nathari ameeleza visa mwenyewe na vingine wahusika wamevielezea. Pia ametumia
mitindo kadha wa kadha. Mfano;Matumizi ya nafsi.
·
Nafsi
ya tatu wingi na umoja:Uk.15
“Peter aliokota kipande cha muhogo” “alisafisha kipande cha muhogo”Uk.27
“walisaidiana wakaubeba” uk.26 “watu walisongamana walisukumana…..”.Kwa
kiasi kikubwa matumizi ya nafsi ya tatu ndiyo yaliyotawala.
·
Nafsi
ya kwanza umoja na wingi:Uk.58
“nitasema nitasema!”Uk.58 “njoo tuongee”Uk.56 “twende tule”.
·
Matumizi
ya nafsi ya pili au dayalojia:Uk.89 pale Mama ntilie alipokumbuka
majibizano yake na Zita.MAMA
NTILIE: na hiyo nguo namna gani? Mbona chafu hivyo na leo ndio
kwanza.Jumanne.PETER: mbwa Mama……ZITA: amenikwaruza kidogo na makucha yake.
·
Matumizi
ya tanzu nyingine za kifasihi, mfano wimbo;Uk.78 “Jua ni moto,Tena ni mwangazaWa
Dunia,Nadina yooNadina mama,Tumwombe Mungu Baba”Uk.10 wimbo alouimba mzee
Lomolomo. “Kuleni nae,Hata bangi vuteni nae,Lakini ni kazi bure,Mwenzenu
nimezaa naye,Pepepe kijani cha mbaazi,Kijaluba na msondoKiboko yao”.
Hivyo mwandishi ametumia mitindo hiyo ili kutomchosha msomaji
mfano wimbo unamburudisha msomaji, majibizano yanavuta umakini zaidi na
matumizi ya nafsi mbalimbali.
MATUMIZI YA LUGHA
Riwaya ya Watoto wa Mama Ntilie imetumia lugha rahisi, fasaha na
inayoeleweka kwa wasomaji. Kuna matumizi ya lugha ya kiingereza mfano.Uk.36 “chloroquine”, “RosewinenaQueenElizabeth”,Uk.83 “faster faster mama” uk.1 “landrover”. Pia kuna matumizi ya lugha ya miitaaniuk.41 “kudeku…..”
Matumizi ya tamathali za
semi
·
Tashibiha:uk.10 “mdomo wake ulio kaa kama bakuli la pombe”Uk.12 “mama
ntilie alikaa kama kapigwa na radi”Uk.15 “miguu kama ya mamba”Uk.46
“aliinamisha shingo nayo ikapinda kama mforosadi” “kichwa kama stafeli”Uk.40.
“kitovu chake kama jicho chongo”Uk.23 “Kurwa aliruka nyuma kama Chui”Uk.45 “akaruka
kama Paa”
·
Tashihisi:Uk. 10 “mabega yenyewe tayari yalikuwa yamechongwa kwa pombe ya
gongo.Yameangalia juu karibu yakutane na masikio”Uk.17 “aliziona nywele za
kipilipili za Musa ngumu kama katani hazijaonja maji walasabuni”Uk.19 “ moshi
wenye harufu ya kuudhi ulilelea hewani na kumlaki mtoto Peter.”Uk.35 “…… visogo
vitatu vilikata kona na kupotea”Uk.46 “koo lilimsaliti”Uk.40 “miguuni raba
zinazocheka kwa huzuni”Uk.46 “mlango ule wa kuungwa na gundi ulitika labeka”
·
Sitiari:Uk.10 “Nyama nyie”Uk.86 “…… wakatembea mwendo wa Farasi”
·
Ritifaa:Uk.38 “Mama? Mama yuko wapi, Baba yuko wapi? Mapenzi yao yako
wapi?”Uk.92 “Zita! Zita! Zita! Zita umekwenda! Umenitoroka, Zita mwanangu”Uk.93
“Baba! Baba watoto? Mwenzangu! Ee! Amka, simama! Usiniachie tanzia hii
peke Yangu”
·
Tafsida:Uk.91 “haja kubwa”
Matumizi ya mbinu
nyingine za kisanaa
·
Onomatopea
/tanakali sauti:Uk.5
“….. aliupinda mgongo kwa mbele akausikia unalia ka-ka-ka-ka, alitema mate
tena Phuuuu”Uk.11 “alikohoa ukho! okho!”Uk.19 “…. Kwa kupiga chafya mbili
au tatu Tcha! Tcha! Tcha!”Uk.50 “Bwee! Bwee! Bwee! Mbwa ….”Uk.50 “Hali …
vicheko Woo! Woo! Weee! Weee! Heheheee! Leooo!”
·
Takriri:Uk.12 “twende! Twende! Nakuwacha nakauwacha!”Uk.58 “ Nivione!
Nivione! Nivione vya kazi gani!”Uk.60 “ Nipishe! Nipishe! Nipishe!Uk.61 “kukurukakara,
kukurukakara,kukurkakara”Uk.91 “ Baba! Baba! amka Baba”
·
Mjalizo:Uk. 40 “… akapata pesa, akala, akashiba”
·
Mdokezo:Uk.58 “usiseme hivyo! Unasikia ee! Usi……”Uk.71mara
akaanza kuimba tena uleule wimbo wake wa “siwezi kuuwa mtu mama”Uk.73 “lakini…….”Uk.79 “
alikumbuka jaa laa jiji na ………”
·
Nidaa:Uk.44 “ Oh! Mungu wangu!”Uk.91 “ Mama wee!”Uk.90 “Hamadi!
Mtume!”
Matumizi ya semi
·
Nahau:Uk.43 “…. Kupiga usingizi”
·
Methali:Uk.34 “ kamba hukatikia pembamba”Uk. 69 “fadhila za Punda”
·
Misemo:Uk.35 “ mtu wa maji” – mlevi.Uk.13 “kwake pombe ya mataputapu na
gongo alivifanya dini”.
Matumizi ya taswira
·
Taswira
mwonekano mfano:Uk.1 “
Mbwa huyu mweusi mwenye mkia mweupe, alionekana akitembea mwendo wa polepole.
Ulimi wake mrefu ulionekana ukidondoka mate ya utelezi” hii inatufanya tupate
picha halisi ya jinsi Mbwa huyo alivyo kupitia maneno ya msanii”.Uk.5 “…..
hatua tatu mbele yake Sufuria, Vikombe na Sahani chafu zilizagaa pale nje
zikimtazama. Akawaona nzi wakitembea na kurukaruka juu ya vyombo vichafu.Uk.10
“ mabega yenyewe tayari yalikuwa yamechonngoka kwa pombe ya gongo yameangalia
juu karibu yakutane na masikio.”Uk.69 “Zenabu alibaki pale mlangoni kavaa gauni
aina ya shifti, kitambaa cha Hariri”
·
Taswira
hisi:Uk.91 “ Mzee Lomolomo
alilala mdomo wazi Nzi wakubwa wa kijani kibichi wamejaa tele mdomoni mwake”.Hii
inamfanya msomaji ajisikie kinyaa kutokana na hali hiyo ya Mzee Lomolomo
anaposema nzi wa kijani kibichi, kwani hao ni nzi wanaokaa sana chooni na
kwenye uchafu.
WAHUSIKA
Mama Ntilie
·
Ni mama mzazi wa Peter na
Zita
·
Ni mke wa Mzee Lomolomo
·
Mlezi mzuri wa familia
·
Ni mvumilivu sana
·
Ana huruma
·
Ni mchapakazi na
anayejituma
·
Ana hali ngumu kimaisha
Mzee Lomolomo
·
Ni mme wa mama ntilie
·
Baba wa Peter na Zita
·
Mlevi
·
Mvivu
·
Si mlezi bora hajali
familia
·
Anakufa kwa sababu ya
kunywa sana pombe
Peter
·
Mtoto wa mama ntilie
·
Anakosa elimu kwa sababu
ya umaskini
·
Ana bidii na mchapakazi
·
Ana huruma
·
Anafungwa jela sababu ya
kufanya biashara haramu ya madawa ya kulevya
Zita
·
Mtoto wa kike wa mama
ntilie
·
Anakosa elimu sababu ya
umaskini
·
Ni mchapakazi
·
Anagombana na Kurwa
hakupenda aje kwao, roho mbaya
·
Anakufa kwa ugonjwa wa
kichaa cha mbwa
Doto
·
Ni mtoto yatima
·
Mtoto wa mtaani
·
Doto anauawa baada ya
kujiingiza katika uhalifu wa wizi
·
Ni mgomvi na katili
Kurwa
·
Ni ndugu yake Doto
·
Anaishi mtaani
·
Ni yatima
·
Ana huruma
·
Ana nguvu na jasiri
·
Ni mchapakazi
·
Anaishia jela kwa sababu
ya makosa ya Musa na Peter
Musa
·
Ni mtoto aliyekosa elimu
baada ya kukosa sare na ada
·
Alikosa malezi mazuri ya
wazazi
·
Mhalifu, anafanya
biashara haramu za madawa ya kulevya
·
Ana tamaa ya pesa
·
Ni rafiki mbaya kwani
alimshauri Peter kuuza madawa ya kulevya
Mwalimu Chikoya
·
Ni mwalimu wa akina Peter
na Zita
·
Aliwafukuza Peter na Zita
shule sababu ya kukosa ada
·
Si mwalimu mzuri
MANDHARI
Mandhari iliyotumika katika riwaya hii ni mandhari ya jiji la
Dar es Salaam. Hii ni kutokana na kutajwa kwa maeneo ya jiji mfano, Manzese,
Tabata, Kiwanda cha Urafiki, Kisutu, Muhimbili nk. Pia ametumia mandhari ya
nyumbani mfano nyumbani kwa Mama Ntilie uk.5, mandhari ya hospitali ya Muhimbili
uk.89, mandhari ya jaani-jaa la Tabata uk.20.
Kwa hiyo mwandishi ametumia mandhari inayosadifu aliyoyaeleza
anaibua dhamira halisi zinazosawiri maisha ya Mtanzania wa leo kwa mandhari
hiyo mfano suala la umaskini na wimbi la watoto wa mitaani.
No comments:
Post a Comment